Home news KUELEKEA MECHI YA KESHO..SIMBA WASHTUKIA HUJUMA..WAHAMA KAMBI YAO YA KIFAHARI YA MBWENI…

KUELEKEA MECHI YA KESHO..SIMBA WASHTUKIA HUJUMA..WAHAMA KAMBI YAO YA KIFAHARI YA MBWENI…

 


DABI ya kesho ina mambo. Simba wamehama kwenye kambi yao rasmi ya Mbweni na kuhamia Upanga ambako ni moja ya makazi ya watu wa Daraja la Juu Jijini Dar es Salaam.

 Walipohama kwa muda ndipo walipotokea wakalala bao 1-0 kwenye mechi dhidi ya Yanga katika Ngao ya Jamii.

Rekodi zinaonyesha tangu Simba wahamie katika kambi yao ya kifahari iliyopo Mbweni wamekutana na Yanga kwenye mechi saba wakitokea hapo na hawajashinda mchezo wowote wa ligi dhidi ya wapinzani wao.

Mechi hizo nne zikiwa za ligi Yanga walishinda mbili na nyingine mbili kumalizika kwa sare.

Michezo mingine mitatu Simba wamekutana na Yanga nje ya ligi ni ule wa fainali ya Mapinduzi Yanga walishinda kwa penalti 4-3, baada ya dakika tisini kumalizika kwa suluhu.

Fainali ya Shirikisho (ASFC) iliyopigwa Kigoma, Simba ndio mchezo pekee alishinda bao 1-0, lililofungwa na Taddeo Lwanga kwa sasa ni majeruhi na hatakuwa sehemu ya kikosi, baada ya hapo mchezo wa Ngao ya Jamii Simba walilala bao 1-0, ambalo lilifungwa na Fiston Mayele anayepewa nafasi ya kuanza Jumamosi.

Licha ya kutotaka kuweka wazi hilo, habari za ndani zinasema kwamba wameamua kuondoka kwa muda kwenye kambi hiyo ili kuangalia upepo mpya. 

Asubuhi ya Jumatano wachezaji na benchi la ufundi la timu hiyo waliondolewa katika kambi yao, wachezaji wote hawakupewa taarifa yoyote ila walishtuka kuna gari mbili aina ya Toyota Coaster, zinawasubiri nje ya jengo kambini kwao tayari kwa safari ya Upanga.

Wamefikia kwenye hoteli iliyopo mitaa ya Kisutu jijini Dar es Salaam inayoitwa City Lodge na wamepigwa marufuku kutoka nje ya geti kwani kila kitu kipo ndani.

KWENDA MAZOEZINI

Katika kuhakikisha wanakwenda na kurudi mazoezini kwa usiri mkubwa wachezaji na benchi la ufundi wanatumia Coaster hizo zenye rangi nyeusi katika vioo na usafiri huo hauna nembo za Simba.

Inaelezwa viongozi wa Simba wameamua kufanya hilo kwa usiri mkubwa kwani wakitumia mabasi yao zile nembo zitakuwa rahisi kugundulika kwamba wanaenda au kutoka mazoezini.

SOMA NA HII  KUHUSU DILI LA KUMSAJILI FEI TOTO...AZAM FC WAANZA KUSHIKANA MASHATI...CEO AMKATAA HADHARANI...

Simba wanafanya mazoezi kwenye shule moja ya kishua iliyopo mitaa ya Upanga na wakiingia ndani ya uwanja hakuna mtu yoyote tofauti na wao mwenye ruhusa ya kuona lolote mpaka watakapoondoka.