Home news KUELEKEA MECHI YA KESHO…NABI AJIONDOA LAWAMANI MAPEMA…ADAI MAKOCHA HAWACHEZI…

KUELEKEA MECHI YA KESHO…NABI AJIONDOA LAWAMANI MAPEMA…ADAI MAKOCHA HAWACHEZI…


KOCHA mkuu wa Yanga, Nassredine Nabi amesema amewasoma wapinzani wake Simba na kujua wanacheza soka la namna gani.

Nabi ameyasema hayo wakati akizungumzia mabadiliko ya makocha kwa Simba baada ya mchezo wa kwanza kikosi hicho kikiongozwa na Didier Gomes na sasa Pablo Franco.

Kocha huyo amesema kwenye mchezo huo hawachezi makocha  bali ni mbinu watakazowapa wachezaji ndio zitacheza.

“Tunajua Simba watacheza vipi na maandalizi tuliyofanya ni kuhakikisha tunachukua pointi tatu kwenye mchezo huu,” amesema Nabi na kuongeza;

“Simba wamecheza mechi ya kimataifa ikiwa ni sehemu nzuri ya maandalizi kwa mchezo huu, mechi itakuwa ngumu”.

Nabi amesema kwenye mchezo huo kila timu ipo nusu kwa nusu kwenye ushindi na kila mmoja anatakiwa apambane ili kupata ushindi.

Kocha huyo amesema kuwa amewaandaa zaidi wachezaji wake kisaikolojia na amekaa nao sehemu moja.

“Maandalizi yapo vizuri na tumekaa sehemu moja ili kujitahidi kuwa kitu kimoja kwenye mchezo huu, tumeweka mitandao yote ya kijamii na lengo likiwa ni kufokasi katika mchezo huu ambao ni muhimu,” amesema Nabi.

Nabi ameongeza akisema;”Ni furaha kubwa kwangu kuwa katika mchezo huu kama kocha lakini pia ni jambo zuri kuiongoza timu kubwa, huu ni mchezo mkubwa  Afrika ni jambo  zuri kuwa sehemu hii.”

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI NA MEMELOD JUMAMOSI HII...SKUDU 'KINYOONGEE' KASEMA HAYA....