Home Uncategorized BALAMA NA NIYONZIMA NDO BAS TENA MSIMU HUU NDANI YA YANGA

BALAMA NA NIYONZIMA NDO BAS TENA MSIMU HUU NDANI YA YANGA


LUC Eymael, Kocha Mkuu wa Yanga, amesema hatakuwa na huduma ya wachezaji wake wawili, Haruna Niyonzima na Mapinduzi Balama ndani ya Yanga mpaka msimu ujao wa 2020/21.
Viungo hao kwa pamoja wamehusika kwenye jumla ya mabao matano ndani ya Yanga katika ligi kuu, Niyonzima akiwa amefunga bao moja, huku Mapinduzi akitupia matatu na asisti moja.

Eymael amesema kuwa viungo hao wanasumbuliwa na majeraha ambayo yatawafanya wakae nje ya uwanja hadi msimu huu unamalizika.

“Niyonzima na Mapinduzi sitakuwa nao kwenye mechi za ushindani zilizobaki kwa sasa mpaka msimu ujao kwa kuwa wanasumbuliwa na majeraha, hivyo ninaamini watakapokuwa fiti watarejea uwanjani kwa ajili ya msimu ujao,” amesema Eymael.
Niyonzima anasumbuliwa na maumivu ya goti, aliyapata kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Biashara United, lakini baadaye akacheza mechi ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam dhidi ya Simba ambapo inaelezwa alisikia maumivu, akatolewa, huku Mapinduzi akiumia kwenye mazoezi wakati Yanga ilipokuwa inajiandaa kucheza na Ndanda.

Kwa sasa, Yanga inajiandaa na mchezo wa ligi dhidi ya Mtibwa Sugar unaotarajiwa kuchezwa Julai 22, Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
SOMA NA HII  KAZE AMKINGIA KIFUA MICHAEL SARPONG