Home Uncategorized NYOTA ANAYEMKIMBIZA KAGERE MDOGOMDOGO ATAJA KINACHOMBEBA

NYOTA ANAYEMKIMBIZA KAGERE MDOGOMDOGO ATAJA KINACHOMBEBA


YUSUPH Mhilu, mshambuliaji namba moja ndani ya Kagera Sugar amesema kuwa siri kubwa iliyojificha kwenye mafaniko yake ni juhudi na kufuata maelekezo ya mwalimu.

Mhilu ametupia jumla ya mabao nane ndani ya ligi akiwa ameachwa kwa mabao manne na kinara wa utupiaji Meddie Kagere wa Simba mwenye mabao 12 ambaye anamfukuzia mdogomdogo.

Akizungumza na Saleh Jembe, Mhilu amesema kuwa kila siku anafanya mazoezi na sala huku nguzo yake kubwa ikiwa ni maelekezo ya mwalimu.

“Mungu kwenye kila kitu na kuamini kwamba ninaweza kupitia maelekezo ambayo napewa na mwalimu, ushirikiano ambao ninapewa ndani ya timu unanifanya niwe bora pia,” amesema.

Kagera Sugar imefunga jumla ya mabao 30, Mhilu amehusika kwenye mabao 10, amefunga nane na kutoa pasi mbili za mabao.

SOMA NA HII  OWEN CHAIMA AMUWAZIA MAKUBWA NCHIMBI WA YANGA