Home Uncategorized POLISI TANZANIA WAIPIGA MKWARA HUU YANGA

POLISI TANZANIA WAIPIGA MKWARA HUU YANGA


UONGOZI wa polisi Tanzania umesema kuwa timu yao ipo vizuri zaidi ya Yanga, itapambana kupata matokeo mbele ya Yanga kwenye mchezo utakaochezwa Uwanja wa Ushirika, Moshi.

Yanga ipo Moshi kwa sasa ikijiaandaa na mchezo wao wa ligi utakaochezwa Februari,18 majira ya saa 10.

Makamu Mwenyekiti wa Polisi Tanzania, Robert Munisi amesema kuwa wanatambua mchezo utakuwa mgumu ila wanajivunia ubora wa timu yao.

“Yanga ni timu kubwa na ina mashabiki wengi kucheza nao kwetu sisi ni kitu kikubwa ukizingatia kwamba muda mrefu hatujacheza nao kwenye mechi za mashindano tutapambana kuonyesha utofauti wetu uwanjani.

“Tunajua kwamba wao wana kikosi bora nasi pia tuna kikosi bora zaidi, kikubwa ni kujipanga na kuona kwamba tunashinda mechi yetu,” amesema.

SOMA NA HII  UHALISIA WA MANARA NA SOKA LA TANZANIA