Home Habari za michezo PAMOJA NA KUFUNGWA JANA….GAMONDI KATIKISA KICHWA KISHA AKASEMA HILI KWA YANGA YAKE…

PAMOJA NA KUFUNGWA JANA….GAMONDI KATIKISA KICHWA KISHA AKASEMA HILI KWA YANGA YAKE…

Habari za Yanga leo

Kocha Mkuu wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans, Miguel Gamondi amesema kikosi chake kipo tayari kwa Michuano ya Kimataifa sambamba na kuanza Ligi Kuu 2023/24.

Gamondi ametoa kauli hiyo akiwa jijini Tanga ambapo kikosi chake kilikuwa na mtihani wa kutetea Ngao ya Jamii, lakini kimeshindwa baada ya kufungwa na Simba SC kwa changamoto ya mikwaju wa Penati jana Jumapili (Agosti 13).

Kocha kutoka nchini Argentina amesema hana wasiwasi na ubora wa wachezaji wake ndani ya kikosi hicho na viongozi wake walimsajilia timu bora yenye vijana wenye njaa na mafanikio.

Ameongeza mechi ambazo wamecheza za kirafiki ukiongeza na zile za michuano ya Ngao ya Jamii zimewasaidia kuboresha ubora wa kikosi hicho na sasa wanawasubiri wapinzani wao KMC FC ambao ndio watafungua nao pazia la ligi.

β€œTunajua sisi ndio watetezi, hivyo kila mmoja liglakinilataka kujua tunaanzaje kwetu tumemaliza maandalizi na sasa tupo tayari kwa mashindano.”

β€œNina furaha na uwajibikaji wa wachezaji katika kipindi chote tulichokuwa kwenye mazoezi tuna wachezaji wanaojua wajibu wao kwa kuanza kushindana kwenye mazoezi, hili ni bora sana.” Amesema Gamondi

Upande wa Kimataifa Young Africans itacheza na Mabingwa wa soka nchini Djibout ASAS Sabieh mwishoni mwa juma hili.

SOMA NA HII  MASHINE INGINE YA KAZI HII HAPA....SIMBA KUMLIPA MSHAHARA KUFRU..., BALEKE, PHIRI BYE BYE...

1 COMMENT

  1. Matumain yetu,,ni,, kuchukua kombe la,,NBC,,na hatupo kichuki Zaid na,,huu ndo mpira ingawa cc wengine ndo maisha yetu ya kutunza familia,,zetu,,,asante coach gamound naamin utafanya mazur Zaid ili kuendelea kumuheshimisha profesa nasridn Nabi,,kupeperusha bendera,,ya cham la WanaπŸ’šπŸ’›πŸ’›πŸ’›πŸ’šπŸ’š