Home Habari za michezo YANGA KUCHEZA NA MIAMBA HAWA ROBO…KIGOGO AKWEA PIPA KUELEKEA MISRI

YANGA KUCHEZA NA MIAMBA HAWA ROBO…KIGOGO AKWEA PIPA KUELEKEA MISRI

Habari za Yanga SC

YANGA imemtuma tena Ofisa Mtendaji wao Mkuu Andre Mtine kufuatilia droo ya Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika sambamba na Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mtine ameondoka nchini leo jioni tayari kwa hafla hiyo itakayofanyika kesho jijini Cairo kuanzia saa 3:30 usiku ambapo Yanga ni moja kati ya 8 zitakazosubiri kujua watakutana na timu ipi kwenye hatua hiyo kwa upande wa shirikisho.

Hii ni mara ya pili kwa Mtine kuhudhuria hafla hiyo ambapo awali alikuwa katika hafla kama hiyo wakati wa kupangwa makundi ya mashindano hayo.

Yanga imefuzu hatua ya robo fainali baada ya kuongoza kundi lao D wakimaliza vinara wa kundi hilo ikiwa ni mara ya kwanza kuongoza makundi katika historia ya klabu hiyo na kesho itaingia mazoezini kuanza maandalizi ya mechi ijayo dhidi ya Geita Gold.

Timu tatu ambazo moja inaweza kungukia kwa Yanga ni USM Alger (Algeria), Pyramids (Misri) na Rivers United (Nigeria) huku Yanga akitarajiwa kuanzia ugenini na kumalizia nyumbani kufuatia kuongoza kundi.

SOMA NA HII  KUHUS BACCA KUTAKIWA MSIMBAZI...YANGA WAIZIMA SIMBA TENA....ISHU NZIMA IKO HIVI...