Home Uncategorized MZUNGU WA SIMBA AJIVUNIA HIKI HAPA KUTOKA KWA WACHEZAJI WAKE

MZUNGU WA SIMBA AJIVUNIA HIKI HAPA KUTOKA KWA WACHEZAJI WAKE

KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck amesema kuwa kurejea kwa nahodha wa Simba John Bocco kunawavuruga wapinzani na kumpa matokeo mazuri ndani ya uwanja.


Bocco alikuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu akitibu majeraha yake ya goti amerejea uwanjani na amefunga mabao matatu na kutoa pasi moja ya bao.

Vanderbroeck amesema:”Kurejea kwa Bocco ni faida kwa timu na kunatoa fursa kwangu kuchagua nani nimuanzishe kati yake pamoja na Meddie Kagere, hawa wakiwa uwanjani wanaleta aina yao ya upekee kwenye kushambulia lango la mpinzani.

“Ninachopenda kuona timu inacheza na kutafuta matokeo kwa sasa hicho ndicho ambacho nimewaambia wachezaji wangu wote, na ninafurahi kuona wanafanya kile kinachotupa matokeo”.
SOMA NA HII  ANGUKO LA YANGA DHIDI YA IHEFU WA KULAUMIWA HUYU HAPA