Home Uncategorized CONTE AKIRI MAMBO MAGUMU SERIE A, JUVENTUS YAISHUSHA NA LAZIO PIA YAWAVUTA...

CONTE AKIRI MAMBO MAGUMU SERIE A, JUVENTUS YAISHUSHA NA LAZIO PIA YAWAVUTA CHINI


ANTONIO Conte, Kocha Mkuu wa timu ya Inter Milan inayoshiriki Seria A ya Italia amesema kuna ugumu wa kupata matokeo kwenye mechi zake kutokana na ushindani uliopo.

Inter Milan jana ilikubali kichapo cha mabao 2-1 mbele ya Lazio, huku Ahley Young akipachika bao la kufutia machozi dakika ya 44.

Kwa upande wa Lazio walipachika mabao yao kupitia kwa Ciro Immobile dakika ya 50 kwa mkwaju wa penalti huku lile la ushindi likifungwa na Sergej Savic dakika ya 69.

Kichapo hicho kinawashusha kileleni na kuipandisha Juventus ambayo imefikisha jumla ya pointi 57 huku Lazio ikiwa nafasi ya tatu na pointi zake 56 na Inter Milan nafasi ya tatu na pointi zake 54.

SOMA NA HII  POLISI TANZANIA US KWA USO NA MTUPIAJI WAO WA ZAMANI ANAYEKIPIGA YANGA