Home Habari za michezo A-Z JINSI IHEFU WALIVYOILIZA YANGA LEO KILAINII KABISA….YA NABI YAMKUTA GAMONDI….

A-Z JINSI IHEFU WALIVYOILIZA YANGA LEO KILAINII KABISA….YA NABI YAMKUTA GAMONDI….

Ihefu vs Yanga

Baada ya kudumu siku 73 katika mechi saba ilizocheza mfululizo Yanga bila kupoteza, hatimaye Ihefu tena imetibua mambo kwa vigogo hao kwa kuwalaza mabao 2-1.

Ihefu inaendelea kuwa ‘mbaya’ wa Yanga kwa msimu wa pili mfululizo baada ya msimu uliopita kuwatibulia walipocheza mechi 49 chini ya aliyekuwa kocha wao, Nassredin Nabi bila kupoteza na kujikuta wakila 2-1 kwenye uwanja wa Highland Estate wilayani Mbarali mkoani Mbeya.

Kabla ya mchezo wa leo Oktoba 4, Yanga ilikuwa imecheza mechi saba mfululizo zikiwamo za kimataifa wakishinda zote, huku wakifunga mabao 20 wakiruhusu moja tu waliporuhusu wavu wao, Agosti 28 dhidi ya AS Djibouti kwenye ushindi wa 5-1 mechi ya klabu bingwa Africa.

Katika mchezo wa leo, ambao ulikuwa mkali na ushindani kwa timu zote, mabao ya timu hizo yamefungwa na Pacome Zouzuoa (Yanga) dakika ya nne na Lenny Kisu akiisawazishia Ihefu dakika ya 40, kisha Charles Ilanfya kuweka la pili dakika ya 65.

Zicheki dondoo za mchezo huu

Ihefu vs YangaBao la Pacome Zouzuoa linakuwa la pili kwake kwenye Ligi Kuu tangu ajiunge na miamba hiyo ya jijini Dar es Salaam mampema msimu huu.

Hii inakuwa mechi ya tisa kwa kocha Miguel Gamond tangu ajiunge na bingwa huyo mtetezi ukiwamo wa Ngao ya Jamii walipopoteza kwa penalti 3-1 dhidi ya Simba kufuatia suluhu ndani ya dakika 90, huku akishinda saba na kupoteza miwili.

Ihefu unakuwa ushindi wake wa pili msimu huu na kufikisha pointi sita walipoichapa Kagera Sugar bao 1-0 huku ikipoteza miwili dhidi ya Geita Gold na Mashujaa FC.

Gamond anakumbana na kilekile kilichomkuta mtangulizi wake, Nabi ambaye naye alikutana na kichapo kama hiho kikiwa cha kwanza akiwa kwenye uwanja huo.

Matokeo hayo yanaifanya Yanga kubaki na pointi zake tisa huku Ihefu ikifikisha sita baada ya timu zote kucheza mechi nne, huku Ihefu ikiendeleza rekodi yake kwa bingwa huyo mtetezi.

SOMA NA HII  KIUNGO WA BURUNDI AJIPIGIA DEBE YANGA...AFUNGUKA ATAKAVYOKIWASHA AKIPANGWA NA FEI TOTO...