Home Habari za michezo MBRAZILI ASHTUKIA JAMBO SIMBA…..AIBUKA NA MSIMAMO HUU KUELEKEA MECHI ZIJAZO…

MBRAZILI ASHTUKIA JAMBO SIMBA…..AIBUKA NA MSIMAMO HUU KUELEKEA MECHI ZIJAZO…

Habari za Simba SC

SIMBA imetua Mkoani Mbeya jana tayari kwa mchezo wao wa kesho dhidi ya wenyeji wao Tanzania Prisons lakini kabla ya safari hiyo kuna mambo matatu mazito ambayo kocha wao Roberto Oliveira ‘Robertinho’ ameyataja matatizo matatu ambayo anapambana nayo.

Kocha Robertinho ameshtukia wachezaji wake kupungua ubora wa nidhamu wakati hawana mpira kama ambavyo wamejionyesha katika mechi zao mbili za Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Power Dynamos ya Zambia ambazo zote walitoka sare.

Robertinho amechukizwa na aina ya mabao ambayo wameyaruhusu dhidi ya Wazambia hao akisema yalikuwa ni mabao rahisi yaliyotokana na baadhi ya wachezaji kutotekeleza vizuri jukumu la kukaba.

“Unaweza kuliangalia bao ambalo tuliruhusu hapa dhidi ya Dynamos, huwezi kuruhusu mtu kufanya maamuzi kama yale wakati mkiwa wengi nyuma kama ambavyo tulifanya hili ni tatizo haliwezi kukubalika tutalifanyia kazi lakini hatutaweza kutoa nafasi ya mchezaji kucheza kama atakuwa hataki kubadilika,” alisema Robertinho.

“Kabla ya kuangalia kosa la mwisho kwa golikipa lakini lazima tuangalie wengine walikuwa na nidhamu gani kabla ya mpira kupigwa na wakati mfungaji anatafuta nafasi, hili ni jambo ambalo tutalifanyia kazi haraka sana.

Ukiacha nidhamu hiyo nyingine ni ile ya kucheza kwa nafasi kulingana na falsafa yao ambayo imekuwa ikiwapotezea utulivu wa kutumia nafasi hasa akiwalenga washambuliaji wao wa mbele.

“Kule mbele nataka kuona tunatumia nafasi za kufunga tatizo ambalo pia tumekuwa nalo lakini hatuwezi kufunga kama tutashindwa kucheza kwa nidhamu ya nafasi, watu wanaona tulikosea kumuingiza John Bocco, kwangu mimi nitamtumia Bocco angalia alivyoingia tulihitaji nidhamu kama yake ya kukaa ndani ya eneo la hatari la wapinzani kwa muda mrefu.

“Alipata nafasi mbili na moja akatumia kutengeneza bao lakini kabla tulikuwa tunapandisha mashambulizi lakini hatukuwa tunakaa maeneo sahihi kuweza kukamilisha mashambulizi yetu.

DAKIKA 180 NGUMU UGENINI

Aidha Robertinho wakati akitua kuwavaa Prisons alisema wana mechi mbili ngumu za ugenini ambazo ugumu utatokana na ratiba ya jinsi gani muda ulivyo karibu kutoka mchezo mmoja kwenda mwingine.

Iko hivi, Simba itacheza Mbeya pale Sokoine kesho Alhamisi Oktoba 5, kisha kutakiwa kusafiri haraka kuanza safari ya kuwafuata Singida Big Stars watakaotakiwa kucheza nao pale Uwanja wa Liti Oktoba 8.

Ugumu ambao Robertinho ameushtukia ni kwamba Simba iwe isiwe lazima wasafiri haraka baada ya mchezo wa Prisons ambao anaamini wachezaji wake watatumia nguvu kubwa kisha kusafiri kwa ndege mpaka jijini Dar es Salaam.

Wakifika Dar es Salaam haraka wanatakiwa kuanza safari ya kuelekea Singida wakipitia Dodoma kisha kusafiri kwa basi kuelekea Singida huku akiona kuna ugumu wa kutofanya mazoezi ndani ya siku mpaka mbili wakati wakisafiri kwenda Singida.

“Ni mechi mbili ngumu ratiba inatubana kwa nafasi kubwa ugumu ninaouona ni kama baada ya mechi ya Prisons tunaweza kukosa mazoezi ya kurudisha miili mpaka tukakapofanya mazoezi ya mwisho kuelekea mchezo dhidi ya Singida.

“Tutaangalia kama kutakuwa na nafasi ya kufanya mabadiliko makubwa ya wachezaji kuanzia mechi moja kwenda nyingine shida nyingine ni baadhi ya majeruhi ambao tunao sasa na vipi kama tukimaliza kucheza na Prisons kama itatokea mwingine akaumia.”

SOMA NA HII  HAWA HAPA SITA WA SIMBA KUIKOSA BIASHARA UNITED