Home Habari za michezo DILI LA ONYANGO LIPO HIVI KUMBE HAKWENDA SINGIDA FOUNTAIN GATE KWA MKOPO...

DILI LA ONYANGO LIPO HIVI KUMBE HAKWENDA SINGIDA FOUNTAIN GATE KWA MKOPO ISHU NZIMA IKO HIVI….

SIMBA juzi imemtangaza rasmi Che Fondoh Malone kuwa Mnyama ili kuchukua nafasi ya Mkenya Joash Onyango, huku awali ikielezwa kwamba ametolewa kwa mkopo kwa Singida Fountain Gate, lakini imebainika dili la beki huyo wa kati halipo kama ilivyoelezwa awali.

Onyango aliyesajiliwa na Simba misimu mitatu iliyopita akitokea Gor Mahia ya Kenya, alikuwa akishinikiza kuondoka klabu hapo tangu kwenye dirisha dogo, kabla ya kuandika tena barua hivi karibuni akisisitiza anataka kusema kwenda kutafuta changamoto mpya kwingine.
Hata hivyo, mabosi wa Simba walimchunia kwanza, ili kuhakikisha inampata mtu sahihi wa kuziba nafasi yake, ndipo baada ya kukamilisha dili la Malone kutoka CotonSport ya Cameroon walikaa tena mezani na kujadiliana kwa kina kabla ya kuafikiana.

Mara baada ya kuvuja kwa picha zilizokuwa zikimuonyesha Onyango akiwa na mmoja wa watu wa Singida, ndipo Simba ilitoa taarifa za kuachana na beki huyo, huku ikielezwa ametolewa kwa mkopo sambamba na mshambuliaji, Habib Kyondo, lakini Mwanaspoti imepenyezewa kwamba dili halipo hivyo.

Ukweli ni kwamba Mkenya huyo amemalizana na mabosi wa Simba baada ya kugoma kutolewa kwa mkopo na kutaka avunjiwe mkataba ili kulamba dili nono kutoka kwa SFG waliomwekea mezani tangu mapema.

Inaelezwa uongozi wa Singida ulimalizana na Onyango kwa kumpa mkataba wa miaka miwili baada ya beki huyo kufikia makubaliano ya kuvunja mkataba na Simba, ili aweze kupata nafasi ya kucheza kimataifa kwani klabu hiyo itashiriki Kombe la Shirikisho Afrika msimu ujao.

Onyango aliyetua Simba, Agosti, 2020 kwa mkataba wa miaka miwili na kuongeza mwingine msimu uliopita unaomalizika katikati ya msimu ujao, aliomba kuondoka kwa hofu ya kukosa namba kikosini.

Chanzo cha karibu kutoka kwa Mkenya huyo kililiambia Mwanaspoti, Onyango amemalizana na Simba kwa kuvunja mkataba na kuingia makubaliano mapya Singida Fountaine Gate.
“Onyango aligoma kutolewa kwa mkopo, kwani alikuwa na ofa nzuri kutoka SFG, hivyo alifanya mazungumzo na Simba ili wamalizane akaanze maisha mapya nje ya klabu hiyo,” kilisema chanzo hicho cha karibu wa beki huyo wa zamani wa Tusker Kenya.
“Kasaini mkataba wa miaka miwili na Singida na jina lake limeingizwa kwenye usajili wa wachezaji watakaocheza Kombe la Shikisho Afrika,” kiliongeza chanzo hicho.

Onyango alipotafutwa, ili afafanue dili zima lilivyo, alisema hana mamlaka ya kulizungumzia, akisema wenye jukumu la kulielezea hilo ni menejimenti yake au Singida.
Kutua kwa Onyango ndani ya Singida kunamfanya aungane na Jonas Mkude, Mohamed Quattara, Victor Akpan, Augustino Okrah, Nelson Okwa, Gadiel Michael, Erasto Nyoni na Beno Kakolanya, Ismael Sawadogo na Kyombo kupewa kwaheri ndani ya Msimbazi.

SOMA NA HII  NAMUNGO WAJIPANGE MBELE YA SIMBA ...... SIO KWA HASIRA