Home Habari za michezo CHAMA, MAYELE WAITEKA CAF….MAJINA YAO YATIKISA AFRIKA NZIMA….

CHAMA, MAYELE WAITEKA CAF….MAJINA YAO YATIKISA AFRIKA NZIMA….

Habari za Simba na Yanga

Kiungo kutoka Zambia na Klabu ya Simba SC Clatous Chotta Chama, ni habari nyingine kutokana na kuhusika kwenye mabao mengi ya kufunga katika Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi wakiwa na alama 9 katika msimamo wa Kundi C.

Mbali na kusepa na mpira pia ana tuzo ya kuwa mchezaji bora katika mzunguuko wanne wa Hakua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Barani Afrika na alipenya kwenye kikosi cha kwanza mchezo wanne pamoja na ule wa tano pamoja na bao lake dhidi ya Horoya AC ambalo lilikuwa ni pigo la faulo kuchaguliwa kuwa bao bora.

Kwa upande wa Yanga mkali wao ni Fiston Kalala Mayele mwenye mabao matatu katika hatua ya makundi Kombe la Shirikisho na ana tuzo ya bao bora dhidi ya US Monastir.

Simba SC ikiwa imefunga mabao 10 baada ya kucheza michezo sita kahusika kwenye mabao matano huku akiwa amesepa na mpira mmoja baada ya kufunga Hat Trick moja.

Chama kawatungua Vipers SC bao moja na Horoya AC mabao matatu na kwenye mchezo huo alitoa pasi moja waliposhinda mabao 7-0 ukiwa ni ushindi mkubwa kwa Simba SC imetupia mabao 9 kwenye hatua ya makundi huku Mayele akihusika kwenye mabao manne kwenye hatua ya makundi msimu kafunga matatu na ana pasi moja huu ya bao.

Mayele anashikilia rekodi ya kuwatungua nje ndani Real Bamako bao mojamoja kwenye michezo miwili mfululizo ni chaguo namba moja la Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi.

SOMA NA HII  SIMBA KUTINGA BUNGENI KUPEWA BARAKA ZA LIGI YA MABINGWA