Home Habari za michezo KUHUSU MKUDE KUTUA SINGIDA….PLUIJM AIBUKA NA HAYA MAPYA….MBRAZILI SIMBA ATOA MSIMAMO…

KUHUSU MKUDE KUTUA SINGIDA….PLUIJM AIBUKA NA HAYA MAPYA….MBRAZILI SIMBA ATOA MSIMAMO…

Habari za Simba

Kocha Mkuu wa Singida Big Stars Hans Pluijm amekanusha taarifa za kuwa kwenye mpango wa kumsajili Kiungo wa Simba SC Jonas Mkude mwishoni mwa msimu huu.

Mkude anatajwa kuwa kwenye mpango wa Kocha huyo, kufuatia Mkataba wake wa Simba SC kitarajia kufikia kikomo mwishoni mwa msimu huu, huku akishindwa kuingia katika kikosi cha kwanza cha Kocha Robertinho.

Kocha Hans ambaye aliwahi kuvinoa vikosi vya Young Africans na Azam FC kwa nyakati tofauti amesema hana mpango wa kumsajili kiungo huyo wa Tanzania, kwa sababu ana wachezaji wengi katika kikosi cha Singida Big Stars ambao wanatosha kupambana na kumpa matokeo.

Amesema anatambua uwezo wa Mkude na anauthamini sana, lakini pia anawaamini sana wachezaji wa Singida Big Stars wanaocheza katika nafasi ya Kiungo, kwa hiyo ni ngumu kwake kufanya maamuzi ya kumsajili.

“Kuna wachezaji wengi Singida kwenye eneo lake kwa hiyo ni ngumu sana kusema nitamchukua, nawaheshimu wachezaji waliopo kwenye kikosi changu, namuheshimu pia Mkude,”

“Mkude anahitaji muda wa kucheza iwe ndani ya nchi ama nje kwake itakuwa sawa, pale Simba kwa sasa ni ngumu kucheza kwani kuna wachezaji wanaofanya vizuri katika nafasi yake.” amesema Pluijm.

Eneo la kiungo la Singida Big Stars yupo Kelvin Nashon na Yusuph Kagoma ambao wote wamesajiliwa kwenye Dirisha Dogo wakitoka kwenye timu ya Geita Gold.

Wakati Kocha Hans akikanusha mpango wa kumsajili Mkude, mwanzoni mwa juma hili Kocha Mkuu wa Simba SC Robertinho alikata mzizi wa fitina kwa kuweka bayana hana shida na kiungo, Jonas Mkude tofauti na uzushi uliopo mtandaoni kwamba wawili hao picha haziivi.

“Wapo wachezaji wengi ambao hawajacheza mechi hivi karibuni na sio Mkude tu, natambua ni mchezaji mzuri na pendwa na amekuwa katika kiwango bora ndani ya Simba kwa muda mrefu.”

“Sina tatizo naye hata kidogo lakini kinachotokea ni aina ya mechi tulizokuwa nazo hivi karibuni na namna tulitaka kuzicheza ndio maana hamjamuona katika orodha,” alisema Robertinho na kuongeza;

“Kama nilivyosema mwanzo, Mkude yupo hapa na umemwona na amekuwa akifanya mazoezi na timu, kinachotokea ni muda kuwa mfinyu wa kuandaa timu na tayari katika eneo lake kuna watu wamecheza kwa ubora na kwa bahatu mbaya zaidi hauwezi kuwatumia wote kwenye mchezo mmoja.”

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI YA KESHO...MTIBWA SUGAR WARUSHA DONGO JINGINE YANGA...WATAMBA KUTIBUA REKODI YAO...