Home Uncategorized MORRISON ATAJWA KUWA TISHIO ZAIDI YANGA, KOCHA AANIKA SABABU

MORRISON ATAJWA KUWA TISHIO ZAIDI YANGA, KOCHA AANIKA SABABU


Luc Eymael, Kocha Mkuu wa Yanga raia wa Ubelgiji, amesema kuwa mchezaji wake Bernard Morrison atafunga mabao mengi kwenye ardhi ya Bongo kutokana na uwezo wake mkubwa wa kushika mambo kichwani na kuyafanyia kazi.

Morrison tangu atue Yanga katika usajili wa dirisha dogo msimu huu, amecheza mechi nne sawa na dakika 360 akitupia mabao mawili na kutoa pasi moja ya bao.

Pasi ya bao aliitoa kwenye mechi ya Ligi Kuu Bara mbele ya Singida United na alizitungua Tanzania Prisons katika mchezo wa Kombe la Shirikisho (FA) na Lipuli mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Eymael alisema; “Ukiachana na ile tabia yake ya kuchezea mpira ambayo niliongea naye na kumwambia aache, Morrison yupo vizuri, unamuona akiwa uwanjani anafunga na anatengeneza nafasi za mabao.

“Basi kama haya anayafanya vzuri tu, unadhani atafunga mabao mangapi mpaka mwisho wa ligi? Namuona akifunga mabao mengi sana. “Kikubwa kwa mchezaji yeyote anayetaka kuwa bora ni lazima afuate kile anacholelekezwa na mwalimu na kufanya mambo ndani ya uwanja,”
SOMA NA HII  HIYO GHARAMA ITAKAYOTEKETEA IWAPO LIGI KUU ENGLAND HAITAKAMILIKA SI MCHEZO