Home Uncategorized UNITED WAONGEZEWA MZIGO KUINASA SAINI YA NAHODHA WA MBWANA SAMATTA

UNITED WAONGEZEWA MZIGO KUINASA SAINI YA NAHODHA WA MBWANA SAMATTA


MANCHESTER United imeonyesha nia ya dhati ya kuipata saini ya nyota wa Aston Villa, Jack Grealish ili kuongeza nguvu dani ya kikosi hicho kwenye kipindi cha usajili majira ya joto.
Grealish ambaye ni nahodha wa Mbwana Samatta amewekwa kwenye hesabu za kutua United kutokana na kuumia kwa nyota wao Marcus Rashford ambaye atakaa nje ya uwanja kwa muda wa miezi sita.
Kwenye Ligi Kuu England, Grealish ametupia mabao saba na pasi tano za mabao jambo linaloifanya United kumuweka namba moja kwa nyota ambao wanawaniwa.
 Kiungo huyo mwenye miaka 24 hakuwa na mpango wa kusepa ndani ya mwezi Januari kwenye klabu hiyo lengo lake lilikuwa ni kuona anatimiza majukumu ndani ya klabu yake anayoipenda kwa kufanya vizuri kwenye ligi pamoja na Kombe la Carabao.
Barcelona na Real Madrid nao pia wameongeza uzito kwenye mchakato wa kinasa saini ya nyota huyo.
SOMA NA HII  EYMAEL - KWA MORRISON TUMEHUJUMIWA