Home Uncategorized YANGA YATUMA UJUMBE HUU KWA MASHABIKI, KAZI YAO NI MOJA TU KIMATAIFA

YANGA YATUMA UJUMBE HUU KWA MASHABIKI, KAZI YAO NI MOJA TU KIMATAIFA


UONGOZI wa Yanga umewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi Septemba14 ili kuwapa sapoti wachezaji wakipambana kwenye mchezo wa hatua ya kwanza na wa kimataifa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Akizungumza na Saleh Jembe, Mratibu wa Yanga, Hafidh Saleh amesema kuwa kwa sasa kikosi kipo vema na kinaendelea na maandalizi kwa ajili ya mchezo huo wa kimataifa.

“Kwa sasa tupo Mwanza na tunaendelea kujipanga kwa ajili ya mchezo wetu wa kimataifa dhidi ya Zesco, tunatambua kwamba haitakuwa kazi nyepesi ila tupo tayari.

“Mashabiki wajitokeze kwa wingi kutupa sapoti na kuwashangilia wachezaji ni jambo la busara na muhimu kwani timu ni yetu sote na lengo letu ni kufanya vizuri,” amesema.

SOMA NA HII  LIPULI YAMCHUNIA MATOLA, KAMBI YAO YAVUNJWA KIMAAJABU