Home Uncategorized JURGEN KLOPP AWATAKA WACHEZAJI WAKE KUPAMBANA NA DUNIA

JURGEN KLOPP AWATAKA WACHEZAJI WAKE KUPAMBANA NA DUNIA

  KOCHA Mkuu wa Liverpool, Jurgen Klopp, amewataka wachezaji wake wapambane dhidi ya dunia huku akisisitiza kwamba timu yake kuwa chini ya kiwango katika mechi za hivi karibuni, hakumuumizi kichwa.

 

Mabingwa hawa wa Premier, hivi karibuni waliambulia pointi mbili tu kati ya tisa ambazo wangeweza kuzipata kwenye mechi tatu na kuiacha vita ya ubingwa kuwa wazi.


Huu umekuwa ni msimu wa kitofauti kwa Klopp ambaye kwa sasa hana mabeki watatu wa kati chaguo la kwanza ambao ni majeruhi.

 

Klopp anafanya mazungumzo na wamiliki Fenway Sports Group, kuhusu changamoto wanazotakiwa kuzikabili katika kipindi cha pili cha msimu lakini amejikita katika kuzungumza na wachezaji wake kuwaongezea morali.

 

“Katika nyakati njema kila mtu hufikiri wamiliki ni watu wazuri sana,” alisema Klopp.


 “Katika nyakati mbaya, kila mtu anafikiri ni wagumu sana. Wanaifuatilia sana klabu, mafanikio ya klabu na jinsi tunavyoyapata.


“Shabiki anaweza akaamini tunahitaji beki wa kati lakini kazi yangu ni kuwafanya imara iwezekanavyo wachezaji tulionao hapa.

 

“Je, beki mmoja wa kati anaweza kumaliza matatizo yetu yote? Klabu inajaribu kufanya inachoweza lakini kama hawawezi tunapaswa kufanya kile tulichokifanya hadi sasa, kuwa imara kama kundi.

 

“Kubaki pamoja na kupambana dhidi ya dunia. Kupambana dhidi ya mazingira yote.Kujibu mashambulizi ya maneno yao kwa kuufanya msimu huu kuwa maalum zaidi ya yote. Hivyo sasa, wakati kila mtu anafi kiri ‘sasa hawana nafasi’, tunawaonye-sha kuwa tunayo.” amesema Klopp.

SOMA NA HII  WENGINE WAWILI WASAINI LEO AZAM FC