Home Uncategorized LIPULI YAMCHUNIA MATOLA, KAMBI YAO YAVUNJWA KIMAAJABU

LIPULI YAMCHUNIA MATOLA, KAMBI YAO YAVUNJWA KIMAAJABU

KOCHA wa Lipuli, Seleman Matola amesema kuwa mpaka sasa hajaitwa mezani na uongozi wa Lipuli kujadili hatma ya mkataba wake pamoja na mipango ya msimu ujao.

Akizungumza na Saleh Jembe, Matola amesema kuwa kambi yao baada ya ligi kuisha pamoja na kumaliza fainali ya kombe la Shirikisho ilivunjwa kwa mtindo wa maajabu.

“Kiukweli namna kambi ilivyovunjwa haikuwa vizuri kwani hakuna mchezaji aliyepata nafasi ya kuonana na uongozi, tumeivunja kambi kwa staili yake.

“Mpaka sasa pia sijaitwa na uongozi wangu kuzungumza nao juu ya hatma yangu na mipango ya msimu ujao hivyo kuhusu Lipuli kwa sasa sijui chochote,” amesema Matola.

SOMA NA HII  HICHI NDICHO KILICHOWAFELISHA SENEGAL AFCON 2019