Home Habari za michezo SHABIKI SIMBA AMJIA JUU MGUNDA…”HANA MAAJABU YOYOTE…YANGA NDIO KIPIMO

SHABIKI SIMBA AMJIA JUU MGUNDA…”HANA MAAJABU YOYOTE…YANGA NDIO KIPIMO

Habari za Simba leo

Shabiki wa Klabu ya Simba, Nabii Meja anasema kuwa Kaimu Kocha Mkuu wa Simba, Juma Mgunda hana maajabu yoyote ndani ya timu hiyo kwa sababu ni ngumu kuibadilisha timu ndani ya wiki mbili.

Mgunda tangu arejee Simba akichukua mikoba ya Benchikha aliyevunja mkataba, amecheza mechi nne akishinda mechi tatu na sare moja huku akifunga mabao 9 na kufungwa mawili jambo ambalo lilikuwa gumu hapo awali.

“Matokeo ya jana tu Simba kucheza vile maneno yamekuwa mengi, unaona Ahmed Ally anavyopost anazugisha mashabiki wasielewe nini wanachokitaka yani tuache ajenda yetu ya kutengeneza timu tuamini Juma Mgunda ni kocha mkali au Simba ni timu kali, hapana. Wachezaji ni walewale, makocha walewale ni sawa na shehe yuleyule kanzu mpya.

“Mgunda hakuna alichokiongeza ni morali tu ya wachezaji kwa sababu kocha ni mpya, wachezaji wanataka waoneshe viwango kwa mwalimu kwa sababu wanaelekea usajili wanataka kupambania namba. Huu ni mzuka tu wa wachezaji.

“Hakuna maajabu aliyoyaonesha Mgunda, huwezi kuibadilisha au kuitengeza timu kwa wiki mbili, hata makocha wa Ulaya hawawezi, Mgunda anaweza kuibadilisha Simba? Guardiola ama Klopp hawezi. Watu wasiojua mpira wataamini Mgunda ameibadilisha Simba. Kwenye kahawa Simba imebadilika kama Real Madrid.

“Angalia mechi ambazo Simba amecheza halafu chukua Yanga mpe zile mechi kisha mpime Mgunda. Yanga ndio kipimo cha Mgunda. Simba wakitaka jambo lao na mechi wakaitaka wanaweza kukupa kitu kikubwa usiamini,” amesema Nabii Меја.

SOMA NA HII  YANGA YAKAMILISHA USAJILI WA KIUNGO HUYU HATARI...ISHU NZIMA HII HAPA