Home Uncategorized MCHUNGAJI MASHIMO, MANARA HAPATOSHI!

MCHUNGAJI MASHIMO, MANARA HAPATOSHI!


MCHUNGAJI wa Kanisa la Emmaus Bible Church, Daudi Mashimo amemtaka Msemaji wa Timu ya Simba, Haji Manara kumuomba radhi msanii Amber Rutty baada ya kumkashfu mitandaoni.

Hivi karibuni, Mashimo alisema Timu ya Simba haiwezi kuwa bingwa, lakini matokeo yakawa kinyume chake ambapo mapaparazi wachokozi walimuuliza Manara anauchukuliaje utabiri wa mchungaji huyo ndipo akasema;

“Akamtabirie Amber Rutty atapiga tena lini zile ‘picha zake’ na kusambaza mtandaoni.”

Kufuatia kauli hiyo, Mashimo alibuka na kucharuka kwa kusema endapo atagoma kumuomba radhi hadharani atafanya maombi ili msemaji huyo augue tumbo la kuendesha mfululizo mpaka atakapomuomba radhi. “Amuombe radhi Amber Rutty vinginevyo ataona,” alisema Mashimo.

SOMA NA HII  KISA MATUSI NA KEJELI SABABU YA SIMBA KUTUPWA NJE CAF, MANA ARA ATOA TAMKO