Home Uncategorized EXCLUSIVE: KAPOMBE ATEMWA RASMI TAIFA STARS

EXCLUSIVE: KAPOMBE ATEMWA RASMI TAIFA STARS


Na George Mganga

Beki wa kulia wa Simba Shomari Kapombe, ametemwa rasmi katika kikosi cha timu ya taifa kutokana na kusumbuliwa na majeruhi.

Kapombe aliumia siku kadhaa zilizopita kwa kujitonesha kidonda chake jambo ambalo lilisababisha Kocha Emmanuel Amunike amuondoe kwenye programu ya mazoezi.

Akizungumza na Radio EFM, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania, Wilfred Kidao, amesema Kapombe hawezi kuwa sehemu ya kikosi cha Taifa Stars, kitakachoondoka leo kuelekea Misri.

Stars inaondoka leo nchini kwenda Misri kwa ajili ya maandalizi rasmi ya michuano ya AFCON 2019.

Kidao amesema wanamtakia kila la kheri Kapombe aweze kutatua changamoto zake zinazomkabili kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania na mashindano mengine.

“Kapombe hawezi kuwa sehemu ya kikosi cha Taifa Stars kinachoondoka leo kwenda Misri.

“Sisi tunamtakia kile la kheri ili aweze kutatua changamoto zake kuelekea msimu unaokuja.”

SOMA NA HII  AZAM FC DARASA KWA WENGINE NDANI YA ARDHI YA BONGO