Home Uncategorized KOCHA YANGA AFAFANUA DAKIKA 15 ZA WAZIR JR

KOCHA YANGA AFAFANUA DAKIKA 15 ZA WAZIR JR

 


KOCHA Msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi amesema kuwa ulikuwa ni mpango maalumu kumuingiza nyota wao Wazir Junior kipindi cha pili na kumtoa baada ya kuyeyusha dakika 15 uwanjani.

Jana Septemba 30, Uwanja wa Azam Complex wakati Yanga ikishinda kwa mabao 2-0 mbele ya KMKM kwenye mchezo wa kirafiki, Junior aliingia kipindi cha pili na alitumia dakika 15 uwanjani kisha akatolewa nafasi yake ikachukuliwa na Farid Mussa.

Akizungumza na Saleh Jembe, Mwambusi amesema kuwa Wazir ni mchezaji wa Yanga na alipewa majukumu maalumu ndani ya dakika ambazo alizitumia ndio maana alipokamilisha kazi yake alitolewa.

“Alipewa kazi maalumu ya kufanya na benchi lilipoona ameweza kutimiza majukumu hayo kwa muda aliopewa alitolewa nje na jukumu lake akapewa mchezaji mwingine.

“Kwa wakati huu bado tupo kwenye kutengeneza timu na ukizingatia mechi ni ya kirafiki hakuna tatizo lolote kila mchezaji ana nafasi yake ndani ya timu na majukumu ni tofauti kabisa, mashabiki waendelee kujitokeza kwa wingi kutupa sapoti,” amesema.


Junior ni ingizo jipya ndani ya Yanga kwa msimu wa 2020/21 ambapo aliibukia ndani ya kikosi hicho akitokea Klabu ya Mbao FC ambayo kwa sasa inashiriki Ligi Daraja la Kwanza.


Msimu wa 2019/20 ndani ya ligi alitupia jumla ya mabao 12 na kuwa miongoni mwa wazawa wenye mabao mengi nyuma ya Meddie Kagere wa Simba ambaye alitupia jumla ya mabao 22. 

Msimu huu bado hajaanza kuonyesha makeke yake ndani ya Yanga kwenye ligi kwa kuwa bado hajapewa majukumu kwenye mechi za ligi kutokana na uwepo wa Michael Sarpong ambaye ndiye mshambuliaji namba moja wa Yanga kwa sasa.


Sarpong kwenye mechi nne za ligi ametupia bao moja kibindoni ilikuwa mbele ya Tanzania Prisons Uwanja wa Mkapa.

SOMA NA HII  REKODI ZA MESSI NA BARCELONA, KWA SASA HATAKI KABISHA KUBAKI HAPO