Home Habari za michezo BALEKE APIGA MKWARA WA MAANA SIMBA….AFUNGUKA KAZI YAKE ILIVYO…

BALEKE APIGA MKWARA WA MAANA SIMBA….AFUNGUKA KAZI YAKE ILIVYO…

Habari za Simba

Straika Jean Baleke juzi alifunga bao la pili katika Ligi Kuu Bara ikiwa na timu wakati Simba ikiifumua Singida Big Stars mabao 3-1, huku akipiga mkwara kwamba kasi aliyonayo sio nguvu ya soda na makipa wa timu pinzani wajiandae tu kuumia ligi ikielekea ukingoni.

Baleke aliyesajiliwa kupitia dirisha dogo, juzi ilikuwa mechi ya tatu tangu ajiunge na Simba baada ya kushindwa kufunga kwenye mechi ya Kombe la ASFC dhidi ya Coastal Union, huku akifunga bao lake la kwanza dhidi ya Dodoma Jiji kwenye mechi ya Ligi Kuu iliyopigwa jijini Dodoma.

Nyota huyo kutoka DR Congo, aliliambia Mwanaspoti anafurahia kuwa na muendelezo mzuri akiamini unazidi kumpa nguvu ya kupambana, kwani ameshajua mashabiki wana imani kubwa na yeye, hivyo anajipanga kufanya makubwa katika mechi zilizosalia kwenye ligi na nyinginezo.

“Kila wakati natamani kuanzia nilipoishia katika michezo iliyopita, raha yangu ni kufunga ama kuhusika kwenye mabao ya timu, katika mechi zilizobaki natamani sana kuonyesha ufundi wa miguu yangu,” alisema Baleke na kuongeza;

“Najua Ligi Kuu ina ushindani, ila kwa vile nimekuja kupiga kazi, nimejipanga vyema kuendelea kutupia nyavuni na kuishi katika malengo niliyonayo kwa timu hii iliyonipa heshima ya kunisajili.”

Baleke alisema hapendi kuzungumza maneno mengi, lakini ni kwamba makipa na mabeki wa timu pinzani ni lazima wajipange, kwa vile amezidi kupata mzuka kuipigania timu.

“Soka ni mchezo wa wazi, sitamani kuzungumza sana, natamani zaidi kazi yangu ndio izungumzwe zaidi, maana nipo Simba timu yenye mashabiki wengi kwa kila ninachokifanya kitaonekana kwa ukubwa zaidi.

“Tuache miguu izungumze kuliko mdomo,” alisema Baleke raia wa DR Congo.

SOMA NA HII  YANGA KILA KITU NI FRESH, BADO WENYE NCHI