Home Uncategorized USHINDI WA REAL MADRID WAAMSHA SHANGWE BONGO NA M-Bet

USHINDI WA REAL MADRID WAAMSHA SHANGWE BONGO NA M-Bet


 USHINDI wa mabao 3-1 wa Real Madrid dhidi ya mahasimu wao, Barcelona ulinogesha chemsha bongo ya kampuni ya michezo ya kubahatisha ya M-Bet Tanzania na mashabiki wa soka kujishindia zawadi mbalimbali.

Tukio hilo lilifanyika kwenye baa ya Tips ya Mikocheni ambapo mbalimbali ya mashabiki kuzawadiwa zawadi mbalimbali zikiwemo jezi orijino za timu hizo mbili, pia waliweza kupiga picha na kombe ‘replica’ la La Liga ambalo Real Madrid ilishinda msimu uliopita.

Mabao ya Real Madrid yalifungwa na  Federico Valverde,Sergio Ramos (kwa njia ya penati) na Luka Modric wakati lile la kufutia machozi la Barcelona lilifungwa na Ansu Fati.

Meneja Masoko wa kampuni ya M-Bet Tanzania, Allen Mushi alisema kuwa wameamua kuwachangamsha mashabiki wa soka ligi ya Hispania kutokana na ushirikiano wao na La Liga.

Mushi amesema kuwa wameamua kuwazawadia mashabiki wa soka kama kutambua mchango wao katika shughuli zao za michezo ya kubahatisha.

Amesema kuwa maswali yao mengi yamelenga ufahamu kuhusiana na La Liga kama mchezaji gani ameyefunga mabao mengi, wachezaji maarufu waliocheza ligi hiyo, mchango wa Cristiano Ronaldo na Lionel Messi katika timu zao, umaarufu wao na makocha.

“M-Bet imeingia mkataba na La Liga katika kuendeleza soka la vijana ili kuleta maendeleo ya soka kwa timu zetu na timu ya Taifa, kabla ya kuanza kuendesha mafunzo mbalimbali, tumeamua kuanza kutoa zawadi kwa mashabiki

Mbali ya mechi ya Clasico, tutaendelea kutoa zawadi katika mechi nyingine mbalimbali za ligi ya Hispania na kutoa elimu ya ufahamu wa ligi hiyo kwa mashabiki wa soka,” amesema.

SOMA NA HII  VIDEO: NYOTA HAWA WA YANGA WATABIRIWA KUSEPA, MOLINGA NDANI