Home Simba SC SIMBA: DODOMA JIJI NI TIMU NGUMU, TUNAWAHESHIMU ILA TUPO TAYARI

SIMBA: DODOMA JIJI NI TIMU NGUMU, TUNAWAHESHIMU ILA TUPO TAYARI


 SELEMAN Matola, Kocha Msaidizi wa Simba amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wao wa kesho dhidi ya Dodoma Jiji utakaochezwa Uwanja wa Mkapa, saa 1:00 usiku.

Matola amesema kuwa wametoka kukamilisha kazi ya kusaka pointi tisa kanda ya ziwa wanareja kuendelea pale ambapo waliishia.

“Tunamshukuru Mungu kwa kuwa tumerejea salama kutoka kanda ya ziwa ambapo huko tulikuwa na kazi ya kusaka pointi tisa na tumezipata pia pointi hizo muhimu.

“Kiujumla kwa sasa kikosi kipo vizuri na wachezaji wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo ambao utakuwa mgumu na ushindani mkubwa, tupo tayari mashabiki watupe sapoti,” amesema Matola.

Walipokutana Uwanja wa Jamhuri, Dodoma ubao ulisoma Dodoma Jiji 1-2 Simba , hivyo mchezo wa kesho unatarajiwa kuwa ni wa kisasi.

Simba inaongoza ligi ikiwa na pointi 58 baada ya kucheza mechi 24 inakutana na Dodoma Jiji ambayo ipo nafasi ya 7 ina pointi 38 na imecheza mechi 27. 

SOMA NA HII  MEDDIE KAGERE: TUTAINGIA NA LENGO MOJA DHIDI YA AS VITA