Home Yanga SC YANGA: UBINGWA BADO SANA, TUSHIKAMANE

YANGA: UBINGWA BADO SANA, TUSHIKAMANE

 HARUNA Niyonzima,  kiungo mshambuliaji wa Yanga amesema kuwa bado wana nafasi ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara kwa kuwa wana mechi nyingi mkononi.

Jana, Aprili 25, ikiwa Uwanja wa Mkapa ilishuhudia inayeyusha pointi tatu jumlajumla kwa ubao kusoma Yanga 0-1 Azam FC. 

Bao pekee la ushindi la Azam FC lilifungwa na Prince Dube ambaye ana mabao 12 akiwa ni kinara wa utupiaji ndani ya Ligi Kuu Bara. 

Niyonzima ambaye alianzia benchi alipata muda wa kuonyesha makeke yake kipindi cha pili ila jitihada zake hazikuleta matunda na kuacha pointi tatu kwenda Azam FC. 

Nyota huyo amesema:” Mchezo ulikuwa mzuri na ni makosa ambayo tunayafanya wapinzani wetu wametumia kutufunga.

“Jambo la msingi tushikamane na sasa ubingwa bado tuna mechi nyingi,”.

Ikiwa imecheza jumla ya mechi 27 imekusanya pointi 57 ipo nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara ina mechi 7 mkononi.

SOMA NA HII  KWA RATIBA HII SASA YANGA WASHINDWE WENYEWE