Home Habari za michezo WAKATI MBRAZILI AKIANZA MAMBO SIMBA…MO DEWJI KAMTAZAMA WEE..KISHA AKAMTAJA MGUNDA..

WAKATI MBRAZILI AKIANZA MAMBO SIMBA…MO DEWJI KAMTAZAMA WEE..KISHA AKAMTAJA MGUNDA..

Habari za Simba

Baada ya kuitembelea kambi Mjini Dubai, Mohamed Dewji ‘Mo’ amemkaribisha Robertinho na kumuahidi Mbrazil huyo kuwa katika dirisha hili la usajili atamuongezea wachezaji wengine wazuri ili aweze kutimiza malengo ya Simba.

“Binafsi nakukaribisha sana Simba, tunaamini uzoefu wako na dhamira yako kwa timu, sisi tutakupa ushirikiano mkubwa na tutakuongezea wachezaji wapya katika dirisha hili la usajili ili uifanye kazi yako kwa usahihi,” amesema Mo.

Katika mazungumzo yake na benchi la ufundi Mo amempongeza na kumshukuru Kocha Juma Mgunda kwa kukubali kuichukua timu katika nyakati ngumu na ameweza kuifanya kuwa imara zaidi.

SOMA NA HII  MNIGERIA ALIYEWATESA YANGA LIGI YA MABINGWA AFRIKA MSIMU ULIOPITA... ATAMBULISHWA AZAM FC KIBABAE....