Home Simba SC MANULA AWAPA MBINU WASUDANI ILI ASAINI DILI JIPYA

MANULA AWAPA MBINU WASUDANI ILI ASAINI DILI JIPYA

 KIPA namba moja wa Klabu ya Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes, Aishi Manula amewapa mbinu mabosi wa Sudan wanaohitaji saini yake namna ya kumpata.

Manula ni miongoni mwa wachezaji ambao watakwea pipa leo kuelekea nchini Misri kuvaana na Al Ahly katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika ambao unatarajiwa kuchezwa Aprili 9.

Katika mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Manula alikaa langoni na hakuruhusu kufungwa na Waarabu hao ambao walipoteza pointi tatu mazima kwa Mkapa.

Amekuwa akitajwa kuwekwa kwenye rada za Al Merrikh ya Sudan ambayo imekuwa ikitajwa kuweka dau la milioni 230 ili kumpata ili akaongeze nguvu katika kikosi hicho ambacho kimeishia hatua ya makundi, Ligi ya Mabingwa Afrika.

Rais wa Al Merrikh, Adam Sudacal amekuwa akitajwa kuwa mstari wa mbele kuongeza nguvu ya kuhitaji saini ya mzawa huyo ambaye ni chaguo namba moja kwa Gomes.

Kuhusu dili hilo Manula amesema:”Nimeskia kuna ofa nyingi juu yangu nami ninaskia furaha kwa kuwa kuna timu ambazo zimevutiwa na huduma yangu.

“Siwezi kwenda popote kwa sasa bila ruhusu ya viongozi wangu kwa sababu mimi sio mchezaji huru bado nina mkataba, ikiwa wanahitaji huduma yangu basi waongee na viongozi” .

SOMA NA HII  KUELEKEA SIMBA DAY YA MWAKA HUU...MKUDE KUENDELEA KUWEKA REKODI HII YA KIPEKEE NCHINI...