Home Yanga SC NYOTA HAWA WATATU WA YANGA KUIKOSA TANZANIA PRISONS LEO

NYOTA HAWA WATATU WA YANGA KUIKOSA TANZANIA PRISONS LEO

 


WACHEZAJI watatu tegemeo hivi sasa wa Yanga viungo Mukoko Tonombe, Feisal Salum ‘Fei Toto’ na mshambuliaji Michael Sarpong wanatarajiwa kuukosa mchezo wa leo Ijumaa dhidi ya Tanzania Prisons.

 

Timu hizo zinatarajiwa kujitupa kwenye Uwanja wa Nelson Mandela, mkoani Rukwa katika mchezo wa Hatua ya 16 Bora ya Kombe la FA.


Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Ijumaa, wachezaji hao wataukosa mchezo huo kutokana na kutumikia adhabu ya kadi za njano.

 

Mtoa taarifa huyo kutoka ndani ya benchi hilo la ufundi ameeleza kuwa nyota hao wanatumikia adhabu ya kadi tatu za njano walizozipata katika michezo iliyopita.


Alisema kuwa Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi anawaandaa wachezaji wengine watakaocheza nafasi zao katika kuelekea mchezo huo.


“Katika kuelekea mchezo wetu wa kesho (leo) tunatarajia kuwakosa wachezaji wetu watatu muhimu ambao ni Tonombe, Fei Toto na Sarpong.


“Watakosekana kutokana na kutumikia adhabu ya kadi tatu za njano walizozipata katika michezo iliyopita ukiwemo uliopita dhidi ya Azam FC.

 

“Kocha hivi sasa yupo katika mipango ya kuwaandaa wachezaji wengine watakaocheza mchezo huo dhidi ya Prisons,” alisema mtoa taarifa.


Alipotafutwa Mkuu wa Kitengo cha Habari cha Yanga, Hassan Bumbuli alithibisha kukosekana kwa wachezaji akisema: “Ni kweli wachezaji hao hawatakuwa sehemu ya mchezo huo kutokana na kutumikia adhabu ya kadi za njano.”

SOMA NA HII  WAKATI NCHIMBI AKITANGAZA KUONDOKA YANGA....UONGOZI WAIBUKA NA KUKANUSHA...WAFICHUA YANYUMA YA PAZIA...