Home Simba SC NYOTA WENGINE SIMBA AMBAO MIKATABA YAO INAKARABIA KUMEGUKA ORODHA HII HAPA

NYOTA WENGINE SIMBA AMBAO MIKATABA YAO INAKARABIA KUMEGUKA ORODHA HII HAPA

IKIWA tayari imeshamalizana na nyota wake watatu ambao ni nahodha John Bocco, nahodha msaidizi Mohamed Hussein,’Tshabalala’ na beki wa pembeni Shomari Kapombe bado nyota wengine mikataba yao inakaribia kufika ukingoni.


Simba chini ya Didier Gomes ambaye ni Kocha Mkuu, inakazi ya kusaka ushindi kesho dhidi ya Kagera Sugar, Uwanja wa Mkapa ambao ni wa Kombe la Shirkisho.

Hawa hapa nyota hao ambao mikataba yao inaweza kumeguka msimu ukikamilika ndani ya ligi 2020/21:-  

Kiungo mkabaji Jonas Mkude. Kipa namba mbili, Beno Kakolanya kiungo mshambuliaji Ibrahim Ajibu beki wa kushoto Gadiel Michael.

Pia kiungo Francis Kahata wengi wanapenda kumuita kijiko na kiungo mshambuliaji Miraji Athumani. Mkongwe Erasto Nyoni ambaye ni kiraka beki wa kati Kenedy Juma na Pascal Wawa.

Kuhusu wachezaji kuondoka ndani ya Simba, hivi karibuni Ofisa Habari wa Simba Haji Manara alisema kuwa mpango wa Simba ni kuwa na wachezaji makini na haitaweza kumuachia mchezaji yeyote ambaye anatakiwa ndani ya kikosi hicho kinachotetea taji la Ligi Kuu Bara pamoja na Kombe la Shirikisho.


SOMA NA HII  MANULA KUIKOSA TENA DABI YA KARIAKOO KISA HIKI HAPA