Home Habari za michezo SIMBA QUEENS MGUU SAWA KUANZA KUITIKISA AFRIKA…CAF YAWABEBA KWENYE RATIBA…

SIMBA QUEENS MGUU SAWA KUANZA KUITIKISA AFRIKA…CAF YAWABEBA KWENYE RATIBA…

Simba Queens itaanza harakati zake za kuutafuta ubingwa wa Afrika kwa kuwavaa wenyeji, ASFAR FC katika mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika utakaofanyika Oktoba 30 kwenye Uwanja wa Prince Heritier Moulay nchini Morocco.

Mashindano hayo yatakayoanza Oktoba 30 hadi Novemba 13 yanashirikisha timu nane ambapo kutoka kundi A ni Simba Queens (Tanzania), ASFAR FC (Morocco), Green Buffaloes (Zambia) na Determine Girls ya Liberia wakati kundi B lina timu za Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, Bayelsa Queens (Nigeria), Wadi Degla FC (Misri) na TP Mazembe ya DR Congo.

Baada ya mchezo huo dhidi ya wenyeji, Simba Queens itashuka tena uwanjani Novemba 2 kwa kuikabili Determine Girls kwenye uwanja huo huo na itamaliza hatua ya makundi kwa kucheza na Green Buffaloes FC Nov. 5 kwenye Uwanja wa Grand Stade De Marrakech.

Simba Queens ilifuzu kucheza Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kutwaa ubingwa wa kanda ya CECAFA kwa kuifunga She Corporates ya Uganda bao 1-0 kwenye mchezo wa fainali. Mabingwa hao wa Ligi Kuu bara ya wanawake hivi sasa wako chini ya kocha raia wa Uganda, Charles Lukula.

SOMA NA HII  MERIDIANBET WAJA NA SHINDANO YA PENATI...CCBRT YAWA WAKWANZA KUNUFAIKA NA THAMANI YA PENATI...