Home Uncategorized KMC YAZIACHA POINTI SITA JUMLA NYANDA ZA JUU KUSINI

KMC YAZIACHA POINTI SITA JUMLA NYANDA ZA JUU KUSINI


TIMU ya KMC imeacha pointi sita jumla ugenini kwenye mechi zake mbili ilizokuwa ikicheza nyanda za juu Kusini.

KMC ilianza kupoteza mbele ya Namungo FC Uwanja wa Majaliwa kwa kufungwa mabao 2-1 kisha ikafuata kupoteza mbele ya Ndanda FC Uwanja wa Nangwanda Sijaona kwa kufungwa mabao 2-1.

KMC imekubali kufungwa mabao manne huku wao wakishinda mabao mawili kwenye mechi mbili walizocheza.

Wafungaji wa mabao ya KMC ni James Msuva na Mohamed Samatta.

Kwenye ushindi wa Ndanda SC wa mabao 2-1 mbele ya KMC FC mabao yalifungwa na Kiggi Makasi  dakika ya 2 na Abdulrazack Ramadhan dakika ya 70 na lile la KMC likifungwa na Mohamed Samatta dakika ya 77

SOMA NA HII  HESABU ZA AZAM FC ZIPO NAMNA HII