Home Uncategorized SIMBA BAADA YA KUMALIZIANA NA BIASHARA SASA HAO KWA STAND UNITED

SIMBA BAADA YA KUMALIZIANA NA BIASHARA SASA HAO KWA STAND UNITED

BAADA ya ushindi wa jana mbele ya Biashara United kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara walioupata Simba, leo kikosi kimeanza safari kuelekea Mwanza.

Simba jana ilishinda mabao 3-1 mbele ya Biashara United mchezo wa Ligi Kuu Bara kitakuwa na mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Stand United Februari 25. 

Safari yao Shinyanga itakuwa kesho Jumatatu, Februari 24 kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo wao wa Kombe la Shirikisho.

Mchezo huo ni hatua ya 16 bora ambapo Simba ilitinga baada ya kuifunga Mwadui FC mabao 2-1 mchezo uliochezwa Uwanja wa Uhuru.

Verified

SOMA NA HII  GAMONDI AFUNGUKA HAYA KUHUSU MCHEZO WAO NA SINGIDA FG