Home Uncategorized KIUNGO LUIS ACHEKELEA KUTUPIA NDANI YA SIMBA, AHADI YAKE HII HAPA

KIUNGO LUIS ACHEKELEA KUTUPIA NDANI YA SIMBA, AHADI YAKE HII HAPA


KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Luis Miquissone amesema kuwa anafurahi kufunga bao lake la kwanza ndani ya Simba na malengo yake ni kuisiaidia timu yake hiyo.

Luis jana kwenye ushindi wa mabao 3-1 Uwanja wa Taifa mbele ya Biashara United alihusika kwenye mabao mawili ambapo alifunga bao la kwanza dakika ya 35 kwa pasi ya Jonas Mkude na alitoa pasi kwa Meddie Kagere huku lile la tatu likifungwa na Francis Kahata.

Luis amesema:-“Ninafurahi kutupia bao ndani ya Simba, kikubwa ambacho nafikiria ni kuona kwamba ninaipa ushindi timu kwa kushirikiana na wachezaji wenzangu na hilo linawezekana,”.

Lusi alijiunga na Simba kwenye usajili wa dirisha dogo msimu huu akitokea timu ya UD Songo.

SOMA NA HII  HILI NDILO BALAA LA MBRAZIL MPYAA ALIYETUA SIMBA, SI WA MCHEZO MCHEZO