Home Habari za michezo MKATABA MPYA WA KIBWANA NA YANGA NI ZAIDI YA KUFRU…KULIPWA MAMILIONI YA...

MKATABA MPYA WA KIBWANA NA YANGA NI ZAIDI YA KUFRU…KULIPWA MAMILIONI YA PESA KAMA ULAYA…


BEKI wa Kulia wa Klabu ya Yanga Kibwana Shomari amesaini mkataba wa miaka mwili kuendelea kuitumikia timu ya wananchi Yanga.

Mkataba wa Kibwana ulikuwa unamalizika mwisho wa msimu huu, hivyo kwa mkataba huo ataendelea kuwatumikia wananchi kwa miaka mingine miwili mbele.

Taarifa za kuongezwa kwa kandarasi ya Kibwana Shomari zimethibitishwa na Klabu ya Yanga kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram.

Inadaiwa kuwa, mkataba huo unamfanya Kibwana kuwa miongoni mwa mastaa wa Yanga wanaolipwa mkwanja wa maana kwa sasa klabuni hapo.

Chanzo cheti ndani ya Yanga, kinaeleza kuwa, Kibwana pamoja na posho, bonasi za mechi pia atakuwa akikunja kibindoni mshahara wa kati ya Milioni 3.5 mpaka 5, kiwango ambacho wachezaji wengi wazawa wamekuwa wakilipwa na klabu hiyo.

Hii ni kusema kwamba, kwa miaka yote miliwi, Kiwabana atakomba mshahara wa milioni kati ya 84 mpaka 120, na hiyo ni nnje ya posho za safari, na bonasi ya timu kushinda mechi mbalimbali na ubingwa wa mashindano ambayo Yanga watashiriki.

SOMA NA HII  WAFALME WA MICHEZO YA KASINO TZ MERIDIANBET...LEO WANAKUJIA NA MCHONGO HUU WA KUTOBOA...