Home Yanga SC NABI ATAJA MAJEMBE SITA MAPYA YANGA

NABI ATAJA MAJEMBE SITA MAPYA YANGA


KOCHA mkuu wa kikosi cha Yanga Nasreddine Nabi ameutaka uongozi wa klabu hiyo kufanya maboresho ya usajili wa nyota wapya wasiozidi sita, kwa ajili ya kutengeneza kikosi bora kitakachoshindana kutwaa mataji kwa msimu ujao wa 2021/22.

Yanga ambao wanakamatia nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi, wamedhamiria kuhakikisha wanarudisha utawala wao katika michuano mbalimbali watakayoshiriki msimu ujao, utawala ambao kwa sasa unaonekana kuchukuliwa na wapinzani wao wa jadi Simba.

Yanga tayari imemalizana na beki wa kulia wa kimataifa wa DR Congo Shabani Djuma, huku pia wakihusishwa kusaka saini ya majina makubwa wakiwemo; Lazarus Kambole, Henock Baka, Marcey Vumbi Ngimbi, Fiston Mayele, na Abubeker Nassir, Anthony Akumu na Heritier Makambo.

Akizungumzia mipango yao ya usajili Ofisa habari wa klabu ya Yanga, Hassan Bumbuli amesema: “Kocha mkuu wa kikosi chetu, Nasreddine Nabi amesema anafurahishwa na ubora wa kikosi tulichonacho, na kuhusiana na maboresho kupitia usajili wa wachezaji wapya, kocha ameutaka uongozi kufanya usajili wa wachezaji watano au sita kwa ajili ya kuongeza nguvu.

“Kocha Nabi hataki kuona tunaondoa wachezaji wengi kwa mara moja kama ambavyo ilitokea kwa misimu miwili iliyopita, hivyo tunatarajia kuachana na baadhi ya wachezaji wakiwemo wanaomaliza mikataba yao, ili kutoa nafasi ya nyota wapya ambao watatangazwa.

SOMA NA HII  AL AHLY WATUA NCHINI KUIKABILI YANGA, WAPOKELEWA NA HAPPY NATION