Home Simba SC MORRISON: TUPO TAYARI DHIDI YA YANGA KWENYE FAINALI SHIRIKISHO

MORRISON: TUPO TAYARI DHIDI YA YANGA KWENYE FAINALI SHIRIKISHO


WINGA wa klabu ya Simba, Bernard Morrison amewaomba msamaha mashabiki wa Simba mara baada ya kupoteza mchezo wao walipocheza na Yanga huku akisema kuwa wapo tayari  kwa ajili ya mchezo wa Fainali ya FA dhidi ya Yanga.

Simba katika mchezo waliocheza dhidi ya Yanga siku ya Jumamosi iliyopita walipoteza kwa kufungwa bao 1-0 katika mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Mkapa Dar es Salaam.

Morrison katika mchezo huo alifanikiwa kucheza kwa dakika zote, licha ya kushindwa kuisaidia timu hiyo kupata matokeo mbele ya Yanga.

Akizungumzia maandalizi yao, Morrison amesema: “Tunawaomba sana msamaha mashabiki wote wa Simba, hatukupanga kupoteza mchezo wetu tuliocheza dhidi ya Yanga, mpira siku zote ndivyo ulivyo, kuna kushinda lakini kuna matokeo mengine mabaya ambayo ni kufungwa au sare.

“Hivyo sisi wachezaji hatukupanga kufungwa na wala hatukupenda iwe hivyo, tuna mechi nyingine tena dhidi ya Yanga ambayo ni ya fainali ya kombe la Shirikisho, sina mengi ya kusema kwa kuwa mchezo bado upo mbali lakini tupo tayari kwaajili ya kupambana.”

SOMA NA HII  KUMBE AHMED LLY ALIKURUPUKA KUHUSU JEZI YA MKUDE.... MAMBO YAPO HIVI JEMEDARI AFUNGUKA KILA KITU