Home Simba SC BOCCO NA MUGALU WAFUNGA MABAO MENGI ZAIDI YA COASTAL UNION

BOCCO NA MUGALU WAFUNGA MABAO MENGI ZAIDI YA COASTAL UNION


NYOTA wawili wa Simba, John Bocco na Chris Mugalu wameipoteza Coastal Union kwa rekodi  matata ya kufunga mabao mengi zaidi ya yale yaliyofungwa na wapinzani wao Coastal Union kwenye mechi zao zote.

Kesho, Julai 11 Simba iliyo nafasi ya kwanza na pointi 76 itakuwa na kazi ya kusaka pointi tatu mbele ya Coastal Union iliyo na pointi 34 inapambana kujinasua kutoka kwenye mstari mwekundu wa kushuka daraja.

Nyota hao wawili wametupia jumla ya mabao 26 baada ya timu hiyo kucheza mechi 31 huku timu ya Coastal Union ya Tanga inayonolewa na Juma Mgunda ikiwa imefunga mabao 21 kwenye mechi 31.

Bocco ametupia mabao 14 akiwa ni mzawa namba moja mwenye mabao mengi huku Mugalu akiwa ametupia jumla ya mabao 12.

Ikumbukwe kwamba walipokutana mchezo wa awali Uwanja wa Sheikh Amri Abeid ubao ulisoma Coastal Union 0-7 Simba na Bocco alisepa na mpira hivyo utakuwa ni mchezo utakaokuwa na ushindani mkubwa.

Mgunda amesema kuwa vijana wake wapo tayari kwa ajili ya ushindani na anaamini kwamba watapata matokeo chanya kwenye mchezo huo.

SOMA NA HII  BAADA YA KUONA MAMBO HAYAELEWEKI ELEWEKI ...WACHEZAJI SIMBA WAANZA KULIA NA HILI...