Home Uncategorized ISHU YA MWAMNYETO KUIBUKIA YANGA, MSIMAMO WA COASTAL UNION UPO HIVI

ISHU YA MWAMNYETO KUIBUKIA YANGA, MSIMAMO WA COASTAL UNION UPO HIVI

 


KOCHA Mkuu wa Klabu ya Coastal Union, Juma Mgunda, amesema kuondoka kwa nyota wao wanne waliokuwa wakitumika kikosi cha kwanza akiwemo aliyekuwa nahodha wa kikosi hicho, Bakari Mwamnyeto, hakuwezi kuwa sababu ya kuifanya klabu hiyo iyumbe, bali ni nafasi kwa vijana wengine ambao watakuja kuifanya klabu hiyo kuwa imara zaidi.

Baadhi ya wachezaji wa Coastal ambao wamekamilisha usajili na kuhamia timu nyingine ni, Bakari Mwamnyeto (Yanga), Ibrahim Ame (Simba) na Ayoub Lyanga (Azam).


Mgunda amesema siku zote falsafa ya Klabu ya Coastal ni kukuza na kulea vipaji, hivyo hawana kizuizi pale wachezaji hao watakapohitajika sehemu nyingine.


“Kwanza mimi kama kocha, najivunia kuona kwa msimu mzima nimeweza kulea vijana ambao wameonyesha kiwango bora kiasi cha kuonekana lulu na klabu nyingine ambazo zinaendelea kuonyesha nia ya kuwahitaji, nami nichukue nafasi hii kuwapongeza na kuwaombea ili waweze kufanya vizuri huko waendako.


“Wengi wamekuwa na hofu kutokana na kuondoka kwa baadhi ya wachezaji nyota wa kikosi chetu akiwemo aliyekuwa nahodha wetu kwa msimu uliopita, Bakari Mwamnyeto lakini ningependa kuwatoa hofu kwani kuondoka kwa mchezaji yeyote hakuwezi kuiteteresha timu yetu bali ni changamoto na nafasi kwa vijana wengine kuweza kufanya bora zaidi,” amesema Mgunda.


Coastal, msimu uliopita ikiwa na mastaa hao, ilimaliza katika nafasi ya saba kwenye msimamo huku ikiwa ni miongoni mwa timu zilizofungwa mabao machache zaidi. Ilifungwa mabao 30 katika michezo 38.

SOMA NA HII  AZAM FC WATIA TIMU MARA KWA WANAJESHI WA MPAKANI