Home Habari za Yanga Leo MWAMNYETO AFUNGUKA KILA KITU…SIMBA YAMFUATA

MWAMNYETO AFUNGUKA KILA KITU…SIMBA YAMFUATA

Habari za Yanga

BAADA ya mchezo wa hisani kati ya Team Mwamnyeto dhidi ya Mbeya All Stars, beki kitasa wa klabu ya yanga anayehusishwa zaidi kutakiwa na Simba alitoa neno baada ya mchezo kumalizika.

Mchezo huo maalumu wa hisani, ulilenga kutafuta fedha kwa ajili ya kusaidia wasiojiweza wakiwamo wagonjwa, yatima, walemavu na masikini kupitia programu ya Mwamnyeto Foundation.

Kaimu Kocha Mkuu wa Simba, Juma Mgunda aliyeinoa timu ya Mwamnyeto, amesema programu kama hizo zinaamsha hamasa kwa wachezaji ambao wanarejesha nguvu kwa jamii kwani baada ya mpira hurudi kwa wananchi.

“Hii ni nzuri sana, kwa sababu hiki kinachofanywa na wachezaji kinapaswa kupewa sapoti kwani baada ya mpira wachezaji hurudi kwao na hakuna cha usimba wala uyanga” amesema Mgunda, nyota wa zamani wa kimataifa aliyewahi kutamba na CDA Dodoma na Coastal Union.

Kwa upande wa Mwamnyeto, mratibu wa programu hiyo, amewashukuru wadau na mashabiki pamoja na wachezaji wenzake walioweza kumsapoti na kwamba kilichopatikana anakirudisha kwa jamii.

“Naenda kujipanga tena mwakani kuboresha pale patakapoonekana mapungufu, lakini kwa ujumla niwashukuru wote waliokuja kunisapoti na kilochopatikana kitaenda kwa walengwa” amesema Mwamnyeto, beki na nahodha wa Yanga anayekipiga pia timu ya taifa na aliyewahi kuwika na Coastal Union.

Bakari Mwamnyeto anahusishwa sana kujiunga Simba baada ya kuwa na ingia toka kwenye kikosi cha Gamondi, pia uongozi wa Simba unahangaika sana kutafuta mbadala wa Henock Inonga ambaye tayari anahusishwa zaidi kujiunga na AS FAR Rabat.

Itakumbwa Simba ndiyo walikuwa wa kwanza kumfuata Mwamnyeto akiwa Coasta Union, kabla ya Yanga kuingilia dili hilo na kumchukua dakika za jioni, ndipo Simba ikamsajili pacha wake Ibrahim Ame ambaye alidumu kwa msimu mmoja tuu Unyamani na kutimkia KMC na kisha baadae Geita Gold, na sasa anakipiga na Mashujaa ya Kigoma.

SOMA NA HII  KUHUSU TIMU KUSUA SUA....DICK JOB AVUNJA UKIMYA YANGA...AFUNGUKA KINACHOWAKWAMISHA...