Home Habari za michezo KUHUSU TIMU KUSUA SUA….DICK JOB AVUNJA UKIMYA YANGA…AFUNGUKA KINACHOWAKWAMISHA…

KUHUSU TIMU KUSUA SUA….DICK JOB AVUNJA UKIMYA YANGA…AFUNGUKA KINACHOWAKWAMISHA…

Habari za Yanga

Nahodha Yanga SC, Dickson Job ameweka wazi ugumu wa mchezo dhidi ya Mashujaa FC baada ya kupata ushindi dakika za majeruhi huku akiweka wazi ugumu wa mchezo ulitokana na kocha wa Mashujaa FC, Abdallah Barres kuwasoma Yanga kwa muda mrefu Uwanjani.

Job amesema hayo baada ya kumalizika kwa mchezo wao dhidi ya Mashujaa FC na Yanga kuibuka na ushindi wa bao 2-1, juzi Alhamisi Februari 8, 2024 katika Dimba la Azam Complex, Chamazi dar es Salaam.

“Pointi tatu za leo (juzi) zina maana kubwa kwetu, ligi ni ngumu na kila timu inafanya vizuri kwa wakati wake hivyo tulizihitaji sana hizi alama tatu ikizingatiwa michezo imekuja miwili lakini yote tumetoka, hii inaongeza morali kwenye timu kuelekea mchezo ujao kule Mbeya dhidi ya Tanzania Prisons.

“Kipindi cha pili nadhani kuna vitu ambavyo mwalimu wao alivisoma sana kutoka kwetu na kuwaekeleza walipoingia vyumbani. Lakini hata sisi kipindi cha pili kuna muda tulipoteza umakini na kufanya mchezo kuwa mgumu upande wetu.

“Kusimama kwa Ligi pia huenda imechangia timu yetu kushuka kidogo kwa sababu ni muda mrefu hatujacheza, kuna ari flani imepotea lakini pia baadhi ya wachezaji hawajatimia kwenye timu ili kutengeneza kombinesheni nzuri, ninaamini wachezaji wote wakirejea timu yetu itasimama na kufanya vizuri,” amesema Job.

SOMA NA HII  KISA KUIFUNGA SANA KILA ANAPOCHEZA NAO....KICHUYA AFUNGUKA ISHU YAKE NA YANGA..."WAACHE KUNILISHA.."