Home Habari za michezo GAMONDI:- HAO TZ PRISONS HATUNA JINSI NAO….WACHEZAJI YANGA NI WACHOVU SANA…

GAMONDI:- HAO TZ PRISONS HATUNA JINSI NAO….WACHEZAJI YANGA NI WACHOVU SANA…

Habari za Yanga SC

Kocha Mkuu wa Klabu ya Yanga, Miguel Gamondi amesema kuwa, amesema kuwa uchovu wa wachezaji na ubovu wa Uwanja wa Sokoine Mbeya unaweza kuufanya mchezo wao dhidi ya Tanzania Prisons ukawa mgumu.

Gamondi amesema hayo wakati akizungumza na wanahabari baada ya kumalizika kwa mchezo dhidi ya Mashujaa FC huku Yanga ikionekana kusua sua kupata matokeo katika michezo yake mitatu iliyocheza ikitoa sare moja na kushinda miwili, ikifunga mabao matatu na kufungwa bao 1.

Katika mchezo huo wa Ligi Kuu ya NBC, uliopigwa katika Dimba la Azam Complex, Chamazi, Yanga iliibuka na ushindi wa bao 2-1, dakika za lala salama.

“Tunajua mechi dhidi ya Tanzania Prisons itakuwa ngumu. Tunafahamu uwanja sio rafiki, wachezaji wana uchovu kutokana na mechi mfululizo lakini tutapambana.

“Ratiba yetu tutaondoka kesho mapema, tutafanya recovering, jambo la mhimu ni kwenda kupambana, ku-enjoy soka na kupata alama tatu, hao Tanzania Prisons nitaanza kuwafikiria kesho,” amesema Kocha Gamondi.

SOMA NA HII  KUHUSU ISHU YA NABI KUSEPA YANGA....MAZITO YAIBUKA...KIGOGO JANGWANI AANIKA A-Z JAMBO LILIVYO...