Home Uncategorized HILI NDILO BALAA LA MBRAZIL MPYAA ALIYETUA SIMBA, SI WA MCHEZO MCHEZO

HILI NDILO BALAA LA MBRAZIL MPYAA ALIYETUA SIMBA, SI WA MCHEZO MCHEZO


MASHABIKI wa Simba wanatamba baada ya usajili wa mshambuliaji Mbrazili, Wilker Henrique da Silva ambaye amesaini mkataba wa miaka miwili ya kukipiga Msimbazi.

Usajili huo unaoendelea kufanywa na Simba, huenda ukawa majibu kwa watani wao wa jadi, Yanga ambao hivi karibuni walifanya usajili wa kishindo kwa kufanikisha saini za wachezaji tisa.

Kupitia akaunti ya mitandao yao ya kijamii, Simba ilimtambulisha Mbrazil huyo ambaye kwa mujibu wa mtandao wa viwango vya usajili duniani kwa wachezaji thamani yake inaonyeshwa kuwa ni Sh mil 206.3.

Mbrazil huyo mwenye umri wa miaka 23, amesaini Simba miaka mawili akitokea Klabu ya Bragantino ya nchini kwao ambaye anafikisha idadi ya Wabrazil wawili ambao tayari wamesajiliwa akiwemo Gerson Fraga anayecheza beki wa kati.

Mshambuliaji anasifa kubwa ya kupiga mashuti, krosi safi na mtulivu akiwa na mpira, jana alitamburishwa na mwenyekiti wa timu hiyo, Swedy Mkwabi mara baada ya kusaini mkataba huo.

Usajili wa Mbrazil huyo anafikisha idadi ya washambuliaji watatu katika kikosi hicho hivyo sasa ataungana na John Bocco na Mnyarwanda, Meddie Kagere katika msimu ujao.

Baadhi ya mitandao ya kijamii inaonyesha kuwa Mbrazil huyo msimu huu amecheza mechi mbili tu na hajafunga bao lolote kwenye Copa do Brasil ambalo hushirikisha timu 91 kutoka sehemu mbalimbali nchini humo.

Katika takwimu za mwaka 2018 katika ligi ya Paulista A3, Mbrazil huyo alicheza mechi 15 na kufunga mabao mawili ikiwa ni wastani wa bao 0.83 kwa mechi huku akipata kadi za njano tatu na nyekundu moja.

Mkwabi alisema kuwa: “Ni kweli tumefanikisha usajili wa Silva ambaye amesaini mkataba wa miaka miwili ya kuichezea Simba.

“Kama tulivyoahidi hivi karibuni kuwa, usajili wetu utaelekeza kwa ajili ya michuano ya kimataifa, hivyo ndiyo sababu ya kumsajili Mbrazili na kati ya nafasi ambazo kocha amezipendekeza ni safu ya ushambuliaji.

“Bado tunaendelea na usajili wetu kwa kuzifanyia maboresho katika kila nafasi ikiwemo hiyo safu ya ulinzi, kiungo na ushambuliaji na kikubwa tunataka kufika Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika,” alisema Mkwabi.

Mbrazili huyo, tofauti na sifa za kupiga mashuti, pia ana mudu kucheza nafasi zaidi ya moja ambazo ni 7, 9, 10 na 11.

SOMA NA HII  NAMUNGO SASA KUKIWASHA MOTO NA YANGA TAIFA