Home epl ARSENAL KAZINI LEO LIGI KUU ENGLAND

ARSENAL KAZINI LEO LIGI KUU ENGLAND


 MIKEL Arteta, Kocha Mkuu wa Arsenal leo atakuwa na kazi ya kuongoza kikosi chake kwenye mchezo wa ufunguzi wa Ligi Kuu England dhidi ya Brenford huku wengi wakiweka wazi kuwa kuna nafasi kubwa ya kocha huyo kufungashiwa virago msimu huu kutokana na timu hiyo kutokuwa na nafasi ya kufanya vizuri ndani ya ligi.

Msimu uliopita Arsenal iliboronga katika Ligi Kuu England na ilikosa nafasi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya na Kombe la Europa jambo ambalo linaongeza presha kwake kuwa katika mazingira magumu ikiwa atashindwa kufanya vizuri msimu huu.

Arsenal inatarajiwa kuvaa uzi wake mpya leo ambao rangi yake ni ya bluu ikiwa ni mara ya kwanza kuonekana wamezivaa katika mchezo wa leo ikiwa itakuwa hivyo katika Uwanja wa Brentford Community. 

Pia Arsenal imepangwa na West Brom kwenye hatua ya pili ya michuano ya Kombe la Carabao huku Aston Villa wao wakiwa wamepangwa na Barrow ambao wanacheza Ligi Daraja la Pili na Leeds watakuwa wakivaana na Crewe.

SOMA NA HII  GUARDIOLA AFURAHIA REKODI YA CITY ULAYA