Home Azam FC WAKATI SIMBA NA YANGA ZIKIKIMBILIA MOROCCO, AZAM WAKIMBILIA HUKU KWA AJILI YA...

WAKATI SIMBA NA YANGA ZIKIKIMBILIA MOROCCO, AZAM WAKIMBILIA HUKU KWA AJILI YA KAMBI


BAADA ya Simba na Yanga kutangaza kuweka kambi ya maandalizi ya msimu ujao nchini Morocco, wababe wenzao Azam wamewakwepa na kupanga kupiga kambi nchini Zambia katika jiji la Ndola.

Awali Azam walikuwa na mapendekezo mawili ya kambi ambapo walipanga kwenda nchi moja kati ya Afrika Kusini na Zambia na kuyachakata na hatimaye huenda siku za hivi karibuni wakasafiri kwenda Zambia sehemu ambayo aliipendekeza kocha mkuu wa timu hiyo, George Lwandamina.

Maandalizi hayo yamepangwa kuanza wiki ijayo kama mambo yataenda vizuri na timu tayari ipo kambini Chamazi, ikijifua tangu Jumatatu ya wiki hii ikisubiri taratibu za kwenda Zambia zikamilike.

Moja ya vigogo wa Azam alidokeza  kuwa wamefunga hesabu kwenye usajili wa wachezaji wa kimataifa na sasa wako kwenye harakati za kunasa nyota wasiozidi watatu wa ndani kisha kwenda Zambia.

“Usajili wa wachezaji wa kigeni tumemaliza, tumebakiza nafasi chache tu za wachezaji wa ndani ambao kwa sasa siwezi kuwataja,” alisema.

SOMA NA HII  AZAM WAIBONYEZA KIZENJI YANGA BONYEEEE....KAZE AWATUPIA MSALA WACHEZAJI..