Home Uncategorized MBELIJIJI WA SIMBA ALETA KIBOKO YA TSHABALALA, KWASI

MBELIJIJI WA SIMBA ALETA KIBOKO YA TSHABALALA, KWASI


BAADA ya kumuongezea mkataba mpya wa miaka miwili ya kuendelea kubaki Simba, uongozi wa timu hiyo umepanga kusajili beki mwingine tishio atakayekuwa mbadala wa Mohammed Hussein ‘Tshabalala’.

Simba inataka kumsajili beki mwingine wa pembeni namba tatu badala ya Mghana, Asante Kwasi ambaye alishindwa kuonyesha ushindani kwa Tshabalala ambaye msimu ujao hatakuwa sehemu ya kikosi hicho.

Timu hiyo, tayari imewaongezea mikataba mipya wachezaji wake sita ambao ni John Bocco, Erasto Nyoni, Aishi Manula, Meddie Kagere, Jonasi Mkude na Tshabalala mwenyewe.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Jumatano, Kocha Mkuu wa timu hiyo tayari ametoa mapendekezo hayo ya kumsajili beki wa pembeni mwenye uwezo na uzoefu wa kucheza michuano ya kimataifa watakayoshiriki mwaka huu katika kukiimarisha kikosi chake.

“Tunataka kuwa na kikosi imara kitakacholeta ushindani mkubwa wa namba katika kila nafasi, hiyo ni baada ya Tshabalala msimu uliopita kukosa mchezaji wa kumpa changamoto.

“Katika nafasi yake alikuwa anacheza na Kwasi ambaye yeye alishindwa kabisa kuonyesha ushindani na badala yake kocha ametoa mapendekezo ya kumsajili beki mwingine mwenye uwezo zaidi ya Tshabalala. ” alisema mtoa taarifa huyo

SOMA NA HII  KMC WATIA TIMU RWANDA, TAYARI KUIVAA TP MAZEMBE