Home Uncategorized SIMBA: YANGA WAISHUKURU GSM BILA WAO KUTUFUNGA INGEKUWA NDOTO

SIMBA: YANGA WAISHUKURU GSM BILA WAO KUTUFUNGA INGEKUWA NDOTO


UONGOZI wa Simba umesema kuwa uongozi wa Yanga ni lazima waushukuru uwepo wa GSM ndani yao kwani isingekuwa hivyo hata kuwachapa kwenye mchezo wao uliochezwa Machi 8 Uwanja wa Taifa ingekuwa ni ndoto.

Yanga iliibuka na ushindi huo kwa bao pekee lililofungwa na Bernard Morrison kwa mpira wa adhabu aliofunga akiwa nje ya 18 na kuwafanya Simba kuyeyusha pointi tatu jumla.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa uwekezaji wa GSM umeipa sapoti kubwa Yanga jambo ambalo limewafanya wawe katika ubora.

“Yanga ni lazima waishukuru GSM kwa kuwa wameweza kuwa kwenye ubora wao, isingekuwa hivyo inakuwa ngumu kabisa kutufunga kwenye mechi ambayo tulicheza nao Machi 8,”.

SOMA NA HII  LEO LIGI KUU BARA RATIBA INAKWENDA KWA MTINDO HUU