Home Uncategorized LIPULI YAPANIA KUFANYA MAAJABU MSIMU UJAO

LIPULI YAPANIA KUFANYA MAAJABU MSIMU UJAO


UONGOZI wa Lipuli umesema kuwa msimu ujao umejipanga kufanya maajabu kwa kupata matokeo chanya.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Lipuli  Clement Sanga amesema kuwa malengo kwa kila timu ni kufanya vizuri nao wamejipanga kuleta ushindani msimu ujao.

“Tupo vizuri na tumejipanga sawa kama ambavyo wengine wanajipanga, tunaamini tutaleta ushindani mkubwa msimu ujao.

“Kwa sasa maandalizi yamepamba moto vijana wanajiweka fiti kuelekea Agosti 23 ambapo ligi inatarajiwa kuanza,” amesema.

Msimu ujao Lipuli itamkosa mchawi wa mipira iliyokufa, Haruna Shamte ambaye ametimkia klabu ya Simba akiwa pamoja na Miraj Athuman.

SOMA NA HII  MGHANA MPYA ASHUSHWA YANGA, SPOTI XTRA LEO JUMAPILI HILI HAPA