Home Uncategorized ISHU YA YANGA KUDAIWA KUMFUTA KAZI KOCHA WA AZAM FC IPO HIVI

ISHU YA YANGA KUDAIWA KUMFUTA KAZI KOCHA WA AZAM FC IPO HIVI


 UONGOZI wa Azam FC umeweka wazi kuwa sababu ya kumfuta kazi Kocha Mkuu Aristica Cioaba sio kufungwa na Yanga, Novemba 25 bao 1-0 Uwanja wa Azam Complex bali ni mchakato ambao ulifanyika kwa muda na kwa utaalamu.

Yanga iliibuka na ushindi wa bao 1-0 mbele ya Azam FC ikiwa Uwanja wao wa nyumbani na kusepa na pointi tatu zilizowapa nafasi ya kukwea kileleni baada ya kuishuhsa Azam FC iliyokuwa kwenye nafasi hiyo kwa muda.


Kwa sasa Yanga ni vinara wana pointi 28 na Azam FC ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 25 zote zimecheza mechi 12.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa wengi wamekuwa wakizungumza kwamba wamemfuta kazi kocha huyo kutokana na kufungwa na Yanga jambo ambalo sio kweli.


“Wengi wamekuwa wakizungumza kwenye mitandao na makundi mbalimbali kwamba tumemfuta kazi Aristica Cioaba kutokana na kufungwa na Yanga hapana hiyo sio kweli.


“Wamekwenda mbali na kuhoji mbona tulifungwa na Simba lakini hatukumfukuza? Hapo jambo ni moja tunaangalia namna wachezaji wanavyocheza, sio rahisi kumfukuza kocha eti kwa sababu umefungwa mechi moja hapana.


“Lakini ikiwa timu itakuwa haipati matokeo ama inapata matokeo kwa tabu hapo kuna tatizo. Tulianza kuitazama timu baada ya kupoteza mbele ya Mtibwa Sugar kuanzia hapo timu haikuweza kucheza vizuri tena.

“Kwenye kila mechi ambayo tulikuwa na kucheza tulikuwa tunafanya uchunguzi na utafiti kujua namna mwendo wetu ulivyo.

“Tumefanya tathimini kwenye mchezo dhidi ya JKT Tanzania tuliopata sare, kisha tukaja kushinda mabao 3-0 dhidi ya Dodoma Jiji, bado timu ilikuwa inapata ushindi ila kwa tabu, ukitazama mpaka tukaja kucheza na KMC mambo yalikuwa ni yaleyale magumu.


“Mchezo wa Yanga nao pia hakukuwa na mchezo mzuri ulikuwa ni mwendelezo wa matokeo mabovu yaliyofanyika kuanzia pale tulipopoteza mbele ya Mtibwa Sugar hivyo hatujakurupuka wala Yanga sio sababu kwetu kumfuta kazi kocha, hayo maneno tu yanaongelewa bila uchunguzi,” amesema.

SOMA NA HII  NYOTA WA MBAO FC ATIMKIA KAGERA SUGAR


Kwa sasa timu ipo chini ya kocha msaidizi Vivier Bahati ambaye atakiongoza kikosi hicho kwenye mechi mbili mbele ya Biashara United na Gwambina FC.